Shukrani tumbi tumbi kwa washika dau na rafiki zangu walionipa hamasa za kuandika Tamthilia hii ya Mbivu Zina Wenyewe...
Shukrani
Nitakuwa mwepesi wa fadhila ikiwa nitakosa kutoa shukrani zangu chekwa chekwa kwa wengi walionipa hamasa katika pilikapilika zangu za kuandika kitabu hiki – Mbivu Zina Wenyewe…
Kwanza, mirathi ya thawabu nashehenia marehemu baba yangu, Mathew Levi Olunga. Hamasa zako zinaishi na nitazidi kuzitumia abadi.
Shukrani zangu za uadilifu, fikra na maono makuu, zamwendea mwandishi mkongwe, Bwana Henry Ole Kulet. Asante sana kwa mchango wako wa hali na mali. Sijui niseme nini. Asante sana!
Mama yangu mjane, Alice Olonga, ndugu zangu John Olonga, Michael Robert Olunga na bila kumsahau Erick Olonga. Ewe Erick, wengi hukusahau katika majukumu mengi lakini kwa uhakika, kiganja chako kilinifikia na mara haba kilikwenda kinywani mwangu. Asante!
Baba yangu mdogo, Mwalimu Noah Olunga. Jamani! Jinsi ulivyonichukua na kunitunza kwa moyo mkunjufu, umekita mizizi. Nimesoma na sasa nimeandika kitabu. Salamu chekwa chekwa nifikishie shangazi na binamu zangu. Ahsante baba!
Pauline Wanyonyi, shukrani sana. Wewe tu ndiye uliyenielewa haswa wakati wenzangu wote walinikwepa kama ukoma. Lo! Sikujua umeimanya lugha hivyo.
Siwezi kukusahau mwalimu wangu Bwana Christopher Wanyama, wa chuo kikuu cha Egerton. Ulinifunza kujua kipaji changu cha kuandika na zaidi ya yote, nimekua kiroho. Mwanzo wa ngoma ni lele, bado tunapambana!
Aaah! Bwana Manoa Mukhwana wa chuo kikuu cha Egerton, mbona nikusahau? Maadamu wewe tu, ndiye uliyeamua kunipa mkono mzito zaidi; angalabu, wa kuhakikisha ya kwamba kitabu hiki kimechapishwa na ndoto yangu imetimia. Ahsante sana! Insafu ya mtu ni mtu na kumpa mtu sio kutupa. Nyasaye akukhonye!.
Diwani mchanga, Joel Gitimu aah! Miaka zinasonga kaka. Uliyonitendea ni mengi ambayo siwezi kusahau. Mola akushehenia tunu tele za tamasha abadi. Inshallah!
Wale sikutaja msikonde, ninawakumbuka kila uchao. Hata hivyo, tukuze lugha na tuzingatie amani na ustaarabu maadamu, wa stara hazumbuki!
AHSANTENI!
OLUNGA RICHARD KARERA
Mwanahamasa mkuu.
(Life coach and motivational speaker)
Digital Educational Theatre.
Nakuru.
Comments