Historia ya Mbivu Zina Wenyewe...

Mwandishi
Mbivu Zina Wenyewe…. ni tamthilia taibu inayozusha mawazo kuhusu tofauti zilizoko baina ya viongozi na wananchi. Inarejelea dhana ya matukio ya vita na ghasia za baada ya uchaguzi. Jinsi wakimbizi wa ndani walivyohangaika na kutaabika. Isitoshe, jinsi taifa nzima lilivyoadhirika. Kimeandikwa hususan kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa vyuo vikuu, shule za upili pamoja na za msingi. Wasomaji wa kawaida pia watanufaika nacho.
Mbunge Bafe, Diwani Ngoho Tataka, Daktari Matimba, Gimbi Juha, Mashaka Wimbi na Mla Hoi, ni washika dau wafisadi katika nchi ya Tabuni. Hii inadhihirika kutokana na matendo yao. Licha ya hayo, Mahakama makuu ya Jinai imewataja kama washukiwa wakuu wa vita na ghasia za baada ya uchaguzi.
Je, mwisho wao utakuwa wapi?
Olunga Richard Karera alizaliwa nchini Kenya mjini Nakuru tarehe 17. 07. 1988. Alipata digrii yake ya (BA in Communication and Media) katika mwaka wa 2011 katika chuo kikuu cha Egerton.
Amewahi kufanya kazi kama mwanahabari na mtangazaji katika redio ya chuo kikuu cha Kenyatta (KU 99.9 FM). Isitoshe, amesimamia tamasha mbalimbali kama Emcee mjini Nakuru. Amehusika katika michezo ya kuigiza katika shule ya upili ya Muhoho na pia Nakuru Playmakers Theatre.
Yeye ni mwanahamasa (Motivational Speaker) wa vijana, wanafunzi wa shule za sekondari, za msingi na hata vyuo. Ni mwandishi maarufu na kazi zake, takriban hamsini, zimechapishwa katika gazeti la Sunday Nation; tangu mwaka (2007). Pia amehudhuria tamasha mbalimbali za uandishi wa insha k.v. la EAC, LRF na CPLC. Ameandika vitabu vingine ambavyo vitatolewa hivi karibuni: Kilio cha Maskini, A Villager in Campus na Makio Will Never Escape.

Comments

News Flash said…
This is a good gesture.
News Flash said…
let us unite and preach peace. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.